Ule utamu wa hadhi ya kibalozi aliyokuwa nayo Dk Wilbroad Slaa, umeyeyuka.
Baada ya kufutiwa hadhi hiyo, sasa atalazimika kurejesha Uhamiaji hati ya kusafiria yenye hadhi ya kidiplomasia.
Hati hiyo inatoa haki ya upendeleo kama vile kusamehewa kodi yeye na familia yake.
Ni hati inayotolewa kwa viongozi wa juu serikalini, watu mashuhuri, wabunge na mabalozi wanaoiwakilisha nchi nje.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Septemba 1, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus ilisema Rais Samia Suluhu Hassan amemvua hadhi ya ubalozi Dk Slaa kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.
Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza sababu za kuvuliwa hadhi hiyo kwa Dk Slaa, aliyeteuliwa kuwa balozi Novemba 23, 2017 na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli.
Rais Magufuli alimteua kuwa Balozi wa Sweden akihudumia pia nchi za Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia, Ukraine na Lithuania.
Ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye hakutaka jina lake kutajwa, amesema Dk Slaa atalazimika kurejesha hati yenye hadhi ya kidiplomasia na atakosa haki zote zinazobebwa na hadhi hiyo.
Amesema kwa kuwa na aina hiyo ya hati ya kusafiria, mmiliki anakuwa na haki ya kinga ya kukamatwa yeye na familia yake anapokuwa nje ya nchi, na haki ya msamaha wa kodi anapofanya ununuzi nje ya nchi

- Category
- NORWEGIAN NEWS
- Tags
- Mwananchi, Thecitizen, Mwanaspoti
Commenting disabled.